KAKA: MABADILIKO YA KATOLIKI: Hujambo! Ninaomba kuichukua fursa hii kupongeza hatua ambayo kanisa katoliki limechukua katika kubadili baadhi ya kauli ambazo zilikuwa zi...
Hujambo? Ninaomba kuichukua nafasi hii kwanza kabisa kuwapongeza ndugu Bitugi Matundura kwa makala yake ya 'Asili ya Kudorora kwa Kiswahili' na Milkah Righa kwa makala yake ya 'Barua kwa Washikadau wa Kiswahili Nchini' ya 06-01-2012. Pili, ni kuwaunga mkono na kujibu baadhi ya maswali mazito yaliyoulizwa na ndugu Milkah Righa. Kudorora kwa Kswahili kote nchini na haswa shuleni, kunachangiwa na mambo mengi. Miongi mwa mambo hayo ni vitabu vya kiada vinavyotumiwa. Ni wazi kuwa Taasisi ya Elimu nchini, imeidhinisha vitabu vingi vinavyotumiwa shuleni. Vitabu vyenyewe vimeandikwa na waandishi mbalimbli ambao wana mitazamo mbalimbali inayokinzana kuhusu kile ambacho wamekiandika. Mifano mizuri ni kuhusu Ngeli za Kiswahili tunazoambiwa kuwa ndio uti wa mgongo wa lugha ya Kiswahili. Waandishi wengi hawana msimamo mmoja wa namna wanavyozianisha na kuzichambua ngeli za Kiswahili.Mathalan, ngeli za A-WA, I-ZI na I-I. Vitabu vingine vinasema kuwa nomino sukari, chumvi,asali, mvua ...
Hujambo? Miezi michache iliyopita, wakenya na ulimwengu kwa jumla, walipokea habari kutoka kwa aliyekuwa mshauri mkuu wa Waziri Mkuu,Raila Odinga katika serikali ya muungano, bw. Miguna Miguna, kuwa alikuwa akikiandika kitabu kumhusu Raila Odinga. Taarifa hizi zilijiri muda mfupi baada yake kupigwa kalamu. Wengi nikiwa mmoja wao, tulisubiri kwa hamu na ghamu kujua alichotaka kukisema bwana Miguna. Hakusikika kwa muda mrefu. Baadaye aliibuka na kutangaza siku rasmi ya kukizindua kitabu chake. Kabla ya kukizindua rasmi, ujumbe uliokuwa ndani ya kitabu hicho chenye anwani Peeling Back The Mask , ulikuwa tayari katika vyombo vya habari. Ilibainika wazi licha ya ujumbe huo kiduchu kuwa yaliyomo hayakuwa ya Mheshimiwa Raila Odinga tu. Pia waliomo na wasiokuwemo serikalini. Siku ya ndovu kumla mwanawe ilikuwa imefika. Wa kualikwa wakaalikwa na wakususia wakafanya hivyo. Vinani! Bwana Miguna hakutishika. Alizindua kitabu chake mbele ya vyombo vya habari na ulimwengu kwa jumla. Wakat...
Hujambo? Tangu gharama ya maisha ianze kukata mbele na nyuma katika matabaka yote kote, Kenya imekuwa ikishuhudia migomo ya wafanyikazi wa umma wakidai haki zao. Kwanza ulikuwa wa walimu, pili, wa wahadhiri na tatu, wa daktari na sasa wafanyikazi wa Posta. Kinachoshangaza ni kwamba, walimu, wahadhiri na daktari walipogoma, hakuna yeyote alipigwa kalamu au aliyepokea vitisho kama hivyo. Baada ya wafanyikazi 600 wa posta kugoma, wamepokea barua za kuwaachisha kazi kwa kudai kuwa mgomo huo haukuwa halali. Swali ni, katiba inaeleza nini kuhusu mgomo? Je, wafanyikazi wa Posta wametendewa haki? Toa maoni yako
Comments
Post a Comment