Posts

Showing posts from January, 2012

KUDORORA KWA KISWAHILI NCHINI

Hujambo? Ninaomba kuichukua nafasi hii kwanza kabisa kuwapongeza ndugu Bitugi Matundura kwa makala yake ya 'Asili ya Kudorora kwa Kiswahili' na Milkah Righa kwa makala yake ya 'Barua kwa Washikadau wa Kiswahili Nchini' ya 06-01-2012. Pili, ni kuwaunga mkono na kujibu baadhi ya maswali mazito yaliyoulizwa na ndugu Milkah Righa. Kudorora kwa Kswahili kote nchini na haswa shuleni, kunachangiwa na mambo mengi. Miongi mwa mambo hayo ni vitabu vya kiada vinavyotumiwa. Ni wazi kuwa Taasisi ya Elimu nchini, imeidhinisha vitabu vingi vinavyotumiwa shuleni. Vitabu vyenyewe vimeandikwa na waandishi mbalimbli ambao wana mitazamo mbalimbali inayokinzana kuhusu kile ambacho wamekiandika. Mifano mizuri ni kuhusu Ngeli za Kiswahili tunazoambiwa kuwa ndio uti wa mgongo wa lugha ya Kiswahili. Waandishi wengi hawana msimamo mmoja wa namna wanavyozianisha na kuzichambua ngeli za Kiswahili.Mathalan, ngeli za A-WA, I-ZI na I-I. Vitabu vingine vinasema kuwa nomino sukari, chumvi,asali, mvua