Posts

Showing posts from July, 2012

MIGUNA MIGUNA MITINI

Hujambo? Miezi michache iliyopita, wakenya na ulimwengu kwa jumla, walipokea habari kutoka kwa aliyekuwa mshauri mkuu wa Waziri Mkuu,Raila Odinga katika serikali ya muungano, bw. Miguna Miguna, kuwa alikuwa akikiandika kitabu kumhusu Raila Odinga. Taarifa hizi zilijiri muda mfupi baada yake kupigwa kalamu. Wengi nikiwa mmoja wao, tulisubiri kwa hamu na ghamu kujua alichotaka kukisema bwana Miguna. Hakusikika kwa muda mrefu. Baadaye aliibuka na kutangaza siku rasmi ya kukizindua kitabu chake. Kabla ya kukizindua rasmi, ujumbe uliokuwa ndani ya kitabu hicho chenye anwani Peeling Back The Mask , ulikuwa tayari katika vyombo vya habari. Ilibainika wazi licha ya ujumbe huo kiduchu kuwa yaliyomo hayakuwa ya Mheshimiwa Raila Odinga tu. Pia waliomo na wasiokuwemo serikalini. Siku ya ndovu kumla mwanawe ilikuwa imefika. Wa kualikwa wakaalikwa na wakususia wakafanya hivyo. Vinani! Bwana Miguna hakutishika. Alizindua kitabu chake mbele ya vyombo vya habari na ulimwengu kwa jumla. Wakat