Posts

Showing posts from 2011

KUH: SHAMRASHAMRA ZA KRISMASI

Hujambo? Katika pitapita zangu za leo 22/12/2011, nimegundua kwamba msongamano wa magari na watu katikati ya jiji la Nairobi, ni wa aina yake. Hali hii ya msongamano imekuwa mbaya zaidi kuliko siku za kawaida za kazi na shule. Kilichonishangaza ni wakati nilipoamua kujitoma katika dukakuu moja mjini. Foleni ndefu za watu zilinifanya kupigwa na butwaa! Angalau kila mmoja alikuwa amenunua bidhaa kadhaa za kutumia 25/12/2011. Miongoni mwa watu hawa walikuwepo waliokuwa wakisafiri mashambani na sehemu nyingine kwenda kusherehekea na jamaa na rafiki. Swali langu ni, hii siku moja 25/12/2011, inastahili kutuhangaisha kwa kiasi hicho?

WAAJIRIWA WA POSTA WAPIGWA KALAMU

Hujambo? Tangu gharama ya maisha ianze kukata mbele na nyuma katika matabaka yote kote, Kenya imekuwa ikishuhudia migomo ya wafanyikazi wa umma wakidai haki zao. Kwanza ulikuwa wa walimu, pili, wa wahadhiri na tatu, wa daktari na sasa wafanyikazi wa Posta. Kinachoshangaza ni kwamba, walimu, wahadhiri na daktari walipogoma, hakuna yeyote alipigwa kalamu au aliyepokea vitisho kama hivyo. Baada ya wafanyikazi 600 wa posta kugoma, wamepokea barua za kuwaachisha kazi kwa kudai kuwa mgomo huo haukuwa halali. Swali ni, katiba inaeleza nini kuhusu mgomo? Je, wafanyikazi wa Posta wametendewa haki? Toa maoni yako

MABADILIKO HAYAJI KWA KUWA VIGEUGEU!

Kila kunapokucha na kuchwa maisha yanazidi kuwa magumu na mazito ya kuweza kuyahimili na kustahimili. Bei ya bidhaa muhimu inaongezeka kwa kasi kama risasi. Anayebaki kulalamika na kunung`unika moyoni ni mwananchi wa kawaida. Iwapo atajaribu kuipaza sauti yake ili iwafikie washikadau, kilio chake huambulia patupu  kwa kupuuzwa na walalahai. Maskini wa Mungu anasalia kupiga dua ili siku moja iwe siku njema. Kufika kwa siku hii huwa ndoto ya alinacha. Kunabaki kuwa sawa na kutarajia kupata maji katika jangwa. Kila wanaposimama hawa walalahoi kuizungumzia hali hii, wanatoa sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta kote ulimwenguni. Sababu ambayo wengine wanaiona kutokuwa ya msingi wowote na kuwaona wao kama wasaliti wa wananchi wao pindi tu wanapoyapata madaraka na mamlaka ya kunyanyasa. Hata hivyo, huenda sisi ndisi waasisi wa baadhi ya matatizo yanayotutatiza. Tumekataa kuwa wakombozi wa taifa letu kwa sababu ya ubinafsi wetu. Mfano mzuri wa hali hii ni pale ambapo ilisemekana kwamba, matai

MABADILIKO YA KATOLIKI

MABADILIKO YA KATOLIKI

KAKA: MABADILIKO YA KATOLIKI

KAKA: MABADILIKO YA KATOLIKI : Hujambo! Ninaomba kuichukua fursa hii kupongeza hatua ambayo kanisa katoliki limechukua katika kubadili baadhi ya kauli ambazo zilikuwa zi...

MABADILIKO YA KATOLIKI

Hujambo! Ninaomba kuichukua fursa hii kupongeza hatua ambayo kanisa katoliki limechukua katika kubadili baadhi ya kauli ambazo zilikuwa zikitumiwa kitambo katika  sala zake. Hatua hii ilitokana na mtazamo kwamba, kauli hizo hazikulandana na zile ambazo lugha ya kilatini ilikuwa imekusudia baada ya kutafsiriwa. Vile vile, ulikuwepo uhitaji mkubwa wa kufanyiwa marekebisho au masahihisho ya tafsiri ya Kingereza na kutafsiriwa kwa Kingereza kinachofaa kwa usanifu wake. Kauli kama ''We believe'' ambayo kwa lugha ya zamani ya kilatini ni credo  kwa maana ya I believe  katika sala ya nasadiki kwa Kiswahili, itabadilika. Kuanzia mwaka wa 2012 itakuwa, "I believe" kutokana na maama asili ya neno lenyewe. Iwapo hatua hii imepigwa kwa lugha ya Kingereza, ningependa pia uchunguzi ufanywe kwa lugha ya Kiswahili  wakati wa sala na ibada za katoliki. Kauli kama '' Mle wote na mnywe wote " wakati wa kipindi cha Ekaristi si Kiswahili sanifu. Kwa lugha ya Kis