MABADILIKO YA KATOLIKI

Hujambo!

Ninaomba kuichukua fursa hii kupongeza hatua ambayo kanisa katoliki limechukua katika kubadili baadhi ya kauli ambazo zilikuwa zikitumiwa kitambo katika  sala zake. Hatua hii ilitokana na mtazamo kwamba, kauli hizo hazikulandana na zile ambazo lugha ya kilatini ilikuwa imekusudia baada ya kutafsiriwa. Vile vile, ulikuwepo uhitaji mkubwa wa kufanyiwa marekebisho au masahihisho ya tafsiri ya Kingereza na kutafsiriwa kwa Kingereza kinachofaa kwa usanifu wake.

Kauli kama ''We believe'' ambayo kwa lugha ya zamani ya kilatini ni credo kwa maana ya I believe katika sala ya nasadiki kwa Kiswahili, itabadilika. Kuanzia mwaka wa 2012 itakuwa, "I believe" kutokana na maama asili ya neno lenyewe.

Iwapo hatua hii imepigwa kwa lugha ya Kingereza, ningependa pia uchunguzi ufanywe kwa lugha ya Kiswahili  wakati wa sala na ibada za katoliki. Kauli kama '' Mle wote na mnywe wote" wakati wa kipindi cha Ekaristi si Kiswahili sanifu. Kwa lugha ya Kiswahili, tunasema, sisi sote, nyinyi nyote na wao wote. Kwa hivyo ni bora kusema, mle nyote au mnywe nyote. Hilo si kosa pekee. Wakati Padri anapomalizia ibada, kauli ya "Nendeni na amani" si Kiswahili bora. Hii ina maana kwamba, watu watakuwa wakienda na amani pia ikienda. Kiswahili sahihi ni "Nendeni kwa amani". Amani hapa ni kama chombo kitakachotumiwa kuenda mahali fulani. Ni sawa na safiri kwa gari, kunywa chai kwa mkate. Ni makosa kusema safiri na gari au kunywa chai na mkate.

Hata hivyo, ninawapongeza wale wote ambao kwao wanatoa michango yao ya kuimarisha na kuboresha lugha ya Kiswahili.

Bonface Andenga
Rununu: 0728570252

Comments

Popular posts from this blog

KUDORORA KWA KISWAHILI NCHINI

MIGUNA MIGUNA MITINI