KUH: SHAMRASHAMRA ZA KRISMASI

Hujambo?
Katika pitapita zangu za leo 22/12/2011, nimegundua kwamba msongamano wa magari na watu katikati ya jiji la Nairobi, ni wa aina yake. Hali hii ya msongamano imekuwa mbaya zaidi kuliko siku za kawaida za kazi na shule.
Kilichonishangaza ni wakati nilipoamua kujitoma katika dukakuu moja mjini. Foleni ndefu za watu zilinifanya kupigwa na butwaa! Angalau kila mmoja alikuwa amenunua bidhaa kadhaa za kutumia 25/12/2011. Miongoni mwa watu hawa walikuwepo waliokuwa wakisafiri mashambani na sehemu nyingine kwenda kusherehekea na jamaa na rafiki.

Swali langu ni, hii siku moja 25/12/2011, inastahili kutuhangaisha kwa kiasi hicho?











Comments

Popular posts from this blog

KUDORORA KWA KISWAHILI NCHINI

MIGUNA MIGUNA MITINI